Siku Niliyojitafakari na Kujipangia Malengo

Leave a Comment 7829 views

Kwenye familia zetu za ki Africa, Sherehe ni kitu muhimu sana, kwa kijiji chetu, sherehe ni sehemu ambayo mtu atajulikana umuhimu wake, na namna anavyokubalika katika jamii. 

Wazee wengi hujipima namna wanavyokubalika katika Jamiii kupitia heshima wanayopewa wakati wa sherehe. 

Ilikuwa mwaka 1994 ambapo ndugu wa jirani wa Mama yangu mzazi, waliazimisha sherehe ya miaka 30 ya ndoa, ndipo walipoandaaa Meza kuu iitwayo High table....  

Kwa utaratibu wa kawaida, ndugu wa jirani kama kaka, dada na mama hukaa kwenye meza kuu kama ndugu wa jirani kwa upendpo na umoja wao. 

Baada ya sherehe kuanza, nilishuhudia Mwenye sherehe ambaye ni kaka wa mama yangu mzazi mwenye sherehe akiondoa kiti alichoandaliwa Mama kwenye meza kuu, na kiti hicho kikasogezwa pembeni na kisha kuondolewa. 

Nilishuhudia Mama akiwa na shamla shamla nyingi akinyamaza ghafla baada ya kuona kiti alichopaswa kukaa kimeondolewa. 

Kisha mama taratibu akasogea nilipokuwa nimeketi kwenye mchanga, akakaaa karibu nami kwa unyonge.  

Nika muuliza, Mama Kila siku unaniambia wale ni ndugu zako kwa nini leo hujakaa nao pamoja......

Mama yangu akanijibu NE NANNI NA MUNU??????, Akimaanisha Je Na mimi ni mtu kati ya watu? 

Kwa utaratibu kabisa, nikasimama nakumuomba tuondoke kwenye sherehe hiyo na sio tuu kuondoka bali, niliingia kwenye banda ambalo nilifunga mbuzi wangu niliyemleta kwenye shere hiyo...... Taratibuuuuuu nikaondoka na mbuzi huyo nikitanguzana na mama kurudi kijijini kwetu yapata umbali wa KM kadhaaa......

Tulipofika Nyumbani Nikamuuliza Mama, Nifanye nini ili na wewe uwe mtu kati ya watu?  Mama yangu akanijibu.... akaniambia Mwanangu.. soma sana uwe padre.. ukiwa padre. Utakuwa na marafiki ulaya..utapanda ndege.. na itaendeleaaaa

www.namsweahouse.com

How to make your first 10K online!

Leave a Comment