Usije kurithishwa Utawala

Leave a Comment 3081 views

Kama Ugali wa ulezi ni afya basi kasheshe yake utaiona pale utakapo enda faraghani ndio somo kubwa nilijifunza, na nikakomaza mikono hadi leo ina malenge lenge... Ilikuwa mwaka mmoja tulipokubwa na njaa kijijini kwenye familia yetu, akili ya kuomba ilisinyaa kabisa, ndipo nikamwambia Baba wenzetu wanapataje chakula sisi tukose? Kuwa mtoto wa mwisho kuna hatari yake, wenzangu wote kipindi hicho wapo mijini, ndio Mzee Kadenge na Mimi Kadenge mdogo, tulipozaam msituni na kazi kubwa huko ilikuwa ni kukata msitu na kutengeneza Ardhi kwa ajili ya kujipatia chakula. 

Ndipo nilipo msikia mzee akisema mimi sitahangaika kupeleka tena mtoto shule unaona kaka zako na dada zako?  Nilikuwa namwangalia nikasema, mzee mimi nitasoma tuu kupitia hili shamba.. Basi nakumbuka mzee akakasirika akaondoka shamba na kuniacha na kipande kikubwa cha kukata matema, alikuwa ni mwenyekiti wa kijiji na mwenyekiti wa chama, alikuwa ni mtu wa kufanya kazi za wananchi ndipo nilipo kutana na mzee mmoja akasema, weee mtoto huyu baba yako anatakurithisha uenyekiti usipo soma.. Nilipata nguvu za ajabu... ndipo siku ya pili nilitoroka na kuendelea na mchakato wa kwenda shule... 

Kasheshe ilikuwa aliponikamata siku ya pili ukizingatia alikuwa mtawala... kesho tutamalizia

Ninajifunza Mengi hapa... Bonyeza hapa chini na usikilize video moja

http://digitalsuccessnow.co.uk/BMwitumba?ty=video-series&ar=system&t=blog29052018

How to make your first 10K online!

Leave a Comment