Kibatali Changu

Leave a Comment 2402 views

Nenda kaombe mafuta ya taa, ndio wimbo uliokuwa wa kila siku, maana sasa lengo la kuwa padre lilianza kukua kwa kasi. Kilicho kuwa kinaniwazisha ni kwamba sasa nikisoma nikawa padre inamaana sitakuwa na watoto?? 

Ilikuwa mwaka 1997 ndipo ndoto za kuwa padre nipate marafiki ulaya zilipopotea kabisa, japo haikuwa rahisi, nilifanya mitiani ya miito, wiki chache baadaye mama alishuka kwenye basi huku akishangilia na kunipa taarifa kuwa nimepata nafasi ya kuwa mwanafunzi wa shule ya dini iliyopo Likonde aka Likonde Seminary School. Niliondoka siku ya pili kwenda parokiani kufuata baraua ya miito, nilichokutana nacho parokiani, nimshituko usio na tija na hivyo kukatisha tamaa ya safari yangu.

Nilikutana na Paroko, nikamweleza nilichofuata, akaniambia oo Benno Jina lako limepelekwa kwenye Kigango chako na usubiri Jumapili utatangaziwa kanisani. Kabla sijaondoka, akafungua barua zilizotaja mahitaji yote muhimu. Akanionyesha jina langu na kuniambia kamwambie mzazi wako ajiandae. 

Siku chache baadaye, nilisikia sikia kwa watu kuwa majina mengine machache tuu ndio wamefanikiwa. 

Safari ya kufuatilia jina langu ilianza hadi parokiani, nikaambiwa niende jimboni, nikafika Jimboni nikaliona Jina langu. 

Ndipo Padre Philbert Mbunda aliponiita na kuniambia, Upadre ni wito, ukiona jina lako lina utata ujue sio kitu utakachofanikiwa nacho. Kwa sababu unauwezo ni bora usubiri majibu ya serikali, na ukifaulu nitakusaidia usome shule za serikali, na kama bado utakuwa na wazo la upadre unaweza kujiunga baada ya kumaliza kidato cha nne. 

Nilianza safari ya kurudi taratibu na nikiwa na maumivu makubwa sana... Siku chache baadaye yakatangazwa matokeo ya wanafunzi walio faulu kwenda shule ya sekondari Ruanda. 

Kutoka Kijiji Kizima cha kindimba Juu shule ya msingi Litundu, Jina moja tuu lilitangazwa, yaaani mwana wa Kadenge aka Benno....ndipo nilipokumbuka Uchungu wa kusoma kwa kutumia kibatali ambacho mafuta ya taa nilikuwa nikiomba omba kwa wafadhiri ambao ...mhhhh mpaka upate koroboi moja ilikuwa ni masimango na maneno...... 

Maandalizi ya kwenda sekondari yakaanza ndipo niliposikia Mzazi wangu akitamka..... Hakuna manufaaa ya kusomesha tena maana hakuona matunda ya waliotangulia..... Ulikuwa ni msiba mwingine ... Nakumbuka Mama alisema, iwe isiwe utasoma tuuu..... mama akasema, mtoto wangu wa mwisho huyu... kijiji kizima amefaulu peke yake.. lazima asome, basi siku hiyo Baba yangu alianzisha vurugu kubwa sana sana.... Ndipo Mama aliposema nnitauza Ng'ombe wangu aliyebaki na mwanangu atasoma.......

Alipotafutwa mteja wa kununua ng'ombe ndipo hali ilipozidi kuwa ya .......... nitaendelea kesho...

Ongeza Ujuzi Wako, Andaa Maisha yako ya Kipato cha Kudumu... Bonyeza hapa

http://digitalsuccessnow.co.uk/BMwitumba?ty=htbs2&t=digitalsuccess30052018

How to make your first 10K online!

Leave a Comment