Na Wewe Unastahili Kusoma Elimu ya Juu

Leave a Comment 10108 views

Nilichelewa kujiunga na masomo ya kidato cha tano, matokeo yalipotangazwa nimefaulu mtihani wa kidato cha nne, ilikuwa ni njema yenye msisimko. Iliyo nikuta kati kati ya kazi ya utengenezaji barabara nikiwa mwendesha mitambo ya choronga barabara.

Ujenzi wa barabara ulishika kasi. Na hii ilikuwa sehemu yangu ya kujidai nikusubiri majibu. 

Habari zilienea kuwa nimefaulu mtihani wa kidato cha nne. Na ndugu zangu waliniita nikakae kwako. Haikuwa safari rahisi pale waliponiambia nenda machimbo katafute pesa ya ada. 

Nikiwa machimbo, majibu yalitoka nimepangiwa Njombe Sekondari.  Haikuwa bahati mbaya, bali ilikuwa ni barua ya wito wa kaka yangu kwenda kumtembelea Jijini Dar es Salaam. 

Ndani ya barua aliandika uje Dar es Salaam ufanye biashara upate ada ya shule. 

Safari ya kutoka msumbiji machimbo ilianza hadi Dar es Salaam. Nilipokelewa na ndipo nilipoanza kushuhudia miujiza ya ndugu.

Nikiwa Dar es Salaam,  niliandikia wito na aliyeniandikia nije Jijini kuwa napaswa kurudi kwa wazee kijijini nikashirikiane nao kupata ada. Hayo yalikuwa maajabu, mwandishi wa barua hiyo alikuwa ndani ya fensi nami nilikuwa nje ya fensi . 

Ilinishitua lakini, nikajipa moyo wa kubaki jijini. 

Katika mahangaiko ya kusaka ada, ndipo nikakumbuka rafiki yangu, mwalimu wangu Mgina wa Shule ya Sekondari aliwahi niambia attachable kufundisha na kwenda kuwa mtaalamu wa Kampuni Mtibwa Sugar.

Nilienda kibanda cha simu, nikakutana na dada Agnes, ndiye aliyenisaidia kupekua namba za simu za mtibwa. 

Sauti ya mgina ikapatikana, ndipo nilipojitambulisha na safari ya madizini kuanza Asubuhi yake. Kwa kuwa nilifanikiwa kumwona ikiwa ni miezi 3 baada ya shule kufunguliwa, basi akasema uende shule nitalipa mahitaji yote moja kwa moja shule..

Nikiwa nimechelewa kabisa kwenda shule.

Sababu ya kukosa mavazi, ndipo nikakusanyiwa mavazi ya watu, na kupewa oversize...

Katika hali isiyo ya kawaida, nilipoingia hapo shuleni. Nilijuta saana, alionekana binti mmoja machachari, aliyeambiwa anipokee na kunionyesha mabweni. 

Kisha anipeleke kwenye bwalo la chakula, binti huyo aliponisogelea akaniuliza, Na wewe ni form five?? 

Akimaanisha mbona mavazi na mwonekano wako hustahili kuwa hapa ulipo... ndipo nilipo mjibu ndio mimi ni form five na yeye atakuwa sehemu ya maisha yangu hadi nakufa. 

Binti huyo ni Mama wa watoto wa nne... Je ndani ya nyumba sasa nimkumbushe usemi huo?

How to make your first 10K online!

Leave a Comment